Simba Sports Club
News

Yussif Basigi Kocha mpya Simba Queens

25 Sep 2024

Basigi raia wa Ghana mwenye umri wa maiaka 52 tayari yupo nchini akiendelea kukisuka kikosi cha Queens.

Basigi anatarajiwa kuanza kuonekana katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.

Basigi ambaye amejiunga nasi akitokea Hasaacas Ladies ya nchini kwao Ghana.

Advertisement

Mwaka 2015 alipata medali ya dhahabu akiwa kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Ghana (Black Queens) ambaye aliiongoza kwenye michuano ya All African Games.

Mwaka 2021 Basigi aliiwezesha Hasaacas Ladies kumaliza nafasi ya tatu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake.

Kocha Mussa Mgosi ataendelea kubaki kuwa Msaidizi wa Basigi kama ilivyokuwa kwa Mgunda.

Back to homepage
Share this story