Yakoub alipata majeraha akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kilichokuwa kinashiriki michuano ya AFCON Disemba mwaka jana nchini Morocco.
Baada ya kukaa nje kwa takribani miezi miwili na nusu Yakoub leo ameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi kabla ya kuruhusiwa kujiunga na wenzake.
Advertisement
Mlinda mlango huyo namba moja wa Taifa Stars ni miongoni mwa wachezaji waliopo jijini Dodoma kwa ajili ya mechi mbili za Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji.