Mchezo huo fainali ulikuwa mkali muda wote huku Simba Asilia itabidi ijilaumu yenyewe baada ya kupoteza nafasi nyingi za kufunga.
Mabingwa hao wapya walipata tiketi ya kuingia fainali baada ya kuwatoa Karume Unstoppable kwa mabao 2-0.
Mabingwa watetezi Simba Damu Fans (SDF) ambao walianzia hatua ya robo fainali walitupwa nje na Wekundu wa Terminal kwa mikwaju ya penati 5-4.
Bonanza hilo ambalo limefana kutokana na mashabiki kujitokeza limeshirikisha timu za matawi na makundi mbalimbali ya wanachama wetu.
Timu zilizoshiriki mashindano hayo ni Kamati ya Roho Mbaya, Wekundu wa Terminal, Simba Ushirikiano, Mpira Pesa, SDF, WhatsApp Makao Makuu, Simba Asilia, Karume Unstoppable, Asili ya Simba, Wekundu wa Kariakoo, Wekundu wa Mtogole, Simba Platinum Supporters na Simba Dar Vibes.