Simba Sports Club
News

Wengine wawili waondoka, mmoja kwa mkopo

6 Jan 2022

Uongozi wa klabu umethibitisha kuachana na wachezaji waliokuwa wetu watatu katika kipindi cha dirisha dogo la usajili kwa makubaliano ya pande zote huku mmoja akitolewa kwa mkopo.

Wachezaji ambao wameondoka kwa makubaliano ni Duncan Nyoni na AbdulSamad Kassim huku mlinda mlango Jeremiah Kisubi akijiunga na Mtibwa Sugar kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

Advertisement

Wachezaji hao wanafanya idadi ya walioondoka kwa makubaliano na klabu kuwa watatu baada ya Ibrahim Ajibu kujiunga na Azam FC, wiki iliyopita.

Katika dirisha hili la usajili tumepanga kufanya mabadiliko kidogo ya kikosi kwa kuongeza wachache na kupunguza pia.

Back to homepage
Share this story