Simba Sports Club
News

Wawa: Hatutacheza kwa presha dhidi ya ASEC

9 Feb 2022

Kauli hiyo imetolewa na mlinzi wa kati, Pascal Wawa ambaye ni raia wa Ivory Coast wanapotoka wapinzani wetu Asec.

Wawa amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora na aina ya uchezaji wa wapinzani lakini tunajiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda.

Wawa ameongeza kuwa wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na watahakikisha wanapambana ili kuhakikisha alama zote tatu zinabaki nyumbani.

Advertisement

"Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Asec ni timu nzuri na ina historia kubwa Afrika lakini tumejipanga na hatutaingia uwanjani kwa presha wala woga.

"Tunafanya maandalizi kama tunavyojiandaa na mechi nyingine. Tunajua umuhimu wa mchezo na tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kubaki na alama tatu nyumbani," amesema Wawa.

Back to homepage
Share this story