Mlinda mlango Ally Salim na mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' wao wamecheza dakika zote 90.
Ally alikuwa muhimili katika kikosi cha Stars huku akiokoa baadhi ya michomo ambayo ilikuwa inaelekea wavuni.
Advertisement
Winga Edwin Balua yeye aliingia akitokea benchi dakika ya 56 na kuipa tabu safi ya ulinzi ya Zambia akitokea upande wa kulia.