Simba Sports Club
News

Watatu kuchuana tuzo ya mchezaji bora mwezi Aprili

29 Apr 2021 By simbasc 14,825 views

Nyota watatu wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao waliongia kwenye kinyang'anyiro hicho ni Clatous Chama, Aishi Manula na Shomari Kapombe ambao mmoja wao atashinda kutokana na idadi ya kura atakazopata.

Wachezaji watano waliingia kwenye kinyang'anyiro hicho lakini Kamati maalumu iliwachuja na kubaki na watatu ambao watapigiwa kura na mashabiki kupitia Tovuti rasmi ya klabu. Nyota wawili ambao walifika hatua hiyo ni Luis Miquissone na Pascal Wawa.

Tuzo hii ambayo inadhaminiwa na Emirate Aluminium Profile itakuwa ni ya tatu kutolewa tangu ilipoanza mwezi Februari mwaka huu.

Advertisement

Mchezaji atakayepata kura nyingi atakabidhiwa tuzo na fedha taslimu Sh 1,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium.

Miquissone alikuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mwezi Februari wakati Joash Onyango alishinda mwezi Machi.

PIGA KURA YAKO HAPA CHINI

[totalpoll id="4058"]
Back to homepage
Share this story