Stars ina mechi mbili muhimu ambazo ikishinda itajihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON ambayo itafanyika nchini Morocco Januari 2025.
Nyota hao walioitwa ni mlinda mlango Aishi Manula, walinzi Shomari Kapombe, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' na Abdulrazack Hamza.
Advertisement
Mwingine aliyejumuishwa kwenye kikosi hicho akiwa ni kiungo mshambuliaji, Kibu Denis.
Kikosi cha Stars kitaingia kambini kesho kujiandaa na mechi hizo ambapo ya kwanza itakuwa ugenini dhidi ya Ethiopia Novemba, 16 na kumaliza nyumbani dhidi ya Guinea Novemba, 19.