Stars itacheza mechi mbili za kufuzu CHAN dhidi ya Somalia ambapo wachezaji wanakiwa kuwasili kambini keshokutwa Ijumaa.
Wachezaji hao ni mlinda mlango Aishi Manula walinzi Mohamed Hussein na Kennedy Juma kiungo Mzamiru Yassin na mshambuliaji Kibu Denis.
Advertisement
Nyota hao hawatakuwa sehemu ya kikosi kitakacho ondoka kesho nchini kuelekea Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu ambapo wataungana na wenzao mara tu wakimaliza majukumu ya timu ya Taifa.