Simba Sports Club
News

Waliokuwa Stars wajiunga na wenzao mazoezini

11 Sep 2023

Nyota hao ni washambuliaji nahodha John Bocco na Kibu Denis kiungo, Mzamiru Yassin na mlinzi, Kennedy Juma.

Kikosi chetu leo kimerejea mazoezini kufuatia mapumziko ya siku moja baada ya mchezo wa kirafiki tuliocheza Jumamosi dhidi ya Ngome na kuibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Advertisement

Tunaendelea na maandalizi ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa Septemba, 16 katika Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola; Zambia.

Back to homepage
Share this story