Wachezaji walifanya mazoezi ya utimamu wa mwili jana (recovery) baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar na baadae wakapewa mapumziko.
Wale walioitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wameruhusiwa kujiunga na wenzao na watarejea baada ya kumaliza majukumu hayo.
Advertisement
Baada ya mapumziko hayo wachezaji watarejea mazoezini kujiandaa na mechi zinazofuata ambapo tunatarajia kupata michezo kadhaa ya kirafiki.