Simba Sports Club
News

Wachezaji wapewa mapumziko ya siku mbili

31 Oct 2022

Kikosi kitarejea tena mazoezini Jumatano Novemba 2 kujianda na mchezo wa Ligi kuu unaofuata dhidi ha Singida Big Stars utakaochezwa Novemba 9, mkoani Singida

Kwa sasa kikosi kitapata muda wa kupumzika kidogo kufuatia ratiba ngumu ya Oktoba lakini benchi la ufundi litaendelea na programu mbalimbali za kiufundi ili kuboresha viwango vya wachezaji.

Advertisement

Kuhusu hali ya majeruhi ndani ya kikosi mpaka sasa ni mlinzi wa kulia Israel Patrick na Jimmyson Mwanuke ndiyo bado wanaendelea kupata matibabu.

Israel anatarajiwa kurudi uwanjani hivi karibuni kutokana na kuendelea vema na matibabu wakati Jimmyson yeye akitarajia kuwa nje kwa muda zaidi.

Back to homepage
Share this story