Simba Sports Club
News

Wachezaji wafanyiwa vipimo vya Covid-19

26 Feb 2022

Baada ya kufika katika Mji wa Berkane wachezaji na benchi la ufundi wamefanyiwa vipimo vya Covid-19 kama inavyoelekezwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Baada ya mlipuko wa Covid-19 kusambaa duniani kote CAF imeweka utaratibu wa kufanya vipimo ili kuzuia maambukizi yasiendelee.

Advertisement

Majibu ya vipimo vya Covid-19 yatatolewa kesho asubuhi, hata hivyo hakuna mchezaji yeyote ambaye ameonyesha dalili ya maambukizi na wote wako kwenye hali nzuri.

Leo usiku kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Manispaa ya Berkane kabla ya kushuka dimbani kesho.

Back to homepage
Share this story