Simba Sports Club
News

Vitomir Vutov Kocha mpya wa makipa

15 Oct 2025

Kabla ya kujiunga nasi Vutov alikuwa akiifundisha timu Litex Lovech ya nchini kwao Bulgaria ambayo aliwahi kuichezea akiwa mchezaji.

Vutov anachukua nafasi ya Wayne Sandilands ambaye aliondoka pamoja na benchi la Kocha, Fadlu Davids.

Advertisement

Uongozi unaendelea kuimarisha benchi la ufundi ili kuweza kumrahisishia kazi Meneja Mkuu, Dimitar Pantev wakati wa kutimiza majukumu yake.

Tayari kocha Vutov yupo jijini Dar es Salaam na amejiunga na kikosi kinachoendelea na maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini utakaopigwa Oktoba 19.

Back to homepage
Share this story