Simba Sports Club
News

Viingilio vya mchezo wetu dhidi ya Mbeya City

16 Jan 2023

Mchezo huo wa ligi ambao ni wa kwanza tangu kuanza kwa mwaka 2023, utapigwa Jumatano saa moja usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huo utakuwa ni wa kwanza kwa Kocha Mkuu Roberto Oliviera 'Robertinho' ambaye atarejea kesho pamoja na kikosi kutoka Dubai tulipoweka kambi ya siku nane.

Mchezo huo pia tutautumia kuwatambulisha wachezaji wetu wapya tuliowasajili katika dirisha la usajili ambalo limefungwa jana.

Viingilio vipo kama ifuatavyo:

Advertisement

Mzunguko Sh 5,000

VIP B na C Sh 10,000

VIP A Sh 15,000

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kupitia mitandao ya simu na vituo pia vimetangazwa.

Back to homepage
Share this story