Simba Sports Club
News

Viingilio mchezo wetu dhidi ya ASEC Mimosas

7 Feb 2022 By simbasc 1,158 views

Jumapili Februari 13 tutashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni kuikabili ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na tayari viingilio vimetangazwa.

Maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri ambapo viingilio hivyo ni kama ifuatavyo;

Mzunguko Sh 5,000

Advertisement

VIP B na C Sh 20,000

VIP A Sh 40,000

Tiketi tayari zimeanza kuuzwa leo kupitia mitandao ya simu na Jumatano tutatangaza vituo ambavyo tiketi zitapatikana.

Back to homepage
Share this story