Simba Sports Club
News Videos

Viingilio mchezo dhidi ya Nsingizini vyatangazwa

21 Oct 2025

Ahmed amesema viingilio hivyo ni rafiki kwa kila Mwanasimba hasa ukizingatia tumemaliza adhabu ya kufungiwa kuingiza mashabiki na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF).

Ahmed ameongeza kuwa tumeupa umuhimu mkubwa mchezo huo kwakuwa tukishinda tutakuwa tumeweka rekodi ya kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya saba.

Ahmed ameongeza kwakusema kuwa tukifanikiwa kuingia hatua ya makundi tutakuwa timu ya tatu baada ya Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambazo zina uhakika wa kuingia hatua hiyo katika kipindi cha karibuni.

"Tumeweka viingilio rafiki ili kila Mwanasimba awezekuja kushiriki kuipeleka timu hatua ya makundi kwa mara ya saba, kikubwa naomba kuwasisitiza tuache vitendo vya vurugu ambazo zitasababisha kufungiwa na kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake," amesema Ahmed.

Hivi hapa Viingilio:

Mzunguko Sh. 5000

Advertisement

VIP C Sh. 10,000

VIP B Sh. 20,000

VIP A Sh. 30,000

Platinum Sh. 150,000

Tanzanite Sh. 250,000

Back to homepage
Share this story