Ukiacha magari yalitoka jijini Dar es Salaam na mashabiki pamoja na Waandishi wa Habari pia njiani tumekutana na Matawi mengine ya Simba ambayo tulijiunga nao hadi Chalinze.
Tulivyofika Chalinze tumepokelewa na msafara wa Bodaboda ambao tulizunguka nao maeneo mbalimbali ya Chalinze mjini.
Advertisement
Balaa zito limefanyika 'Round About' ya Chalinze ambapo magari, Bodaboda pamoja na mashabiki waliokuwa wanatembea kwa miguu walikuwa wakishangilia wakiongozwa na watu wa hamasa.