Simba Sports Club
News

VIDEO: Timu yafanya mazoezi ya mwisho TTC Mtwara

6 May 2023

Mchezo wetu wa kesho utaanza saa 9:30 Alasiri katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona ambapo tunaamini utakuwa mgumu.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri, hakuna yoyote ambaye tutamkosa kutokana na kupata maumivu.

Advertisement

Kocha mkuu Robertinho pamoja na wasaidizi wake watakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi sababu wachezaji wote wapo tayari.

Baada ya kukamilika kwa mazoezi tulienda kutembelea Uwanja wa Nangwanda Sijaona (feel the pitch) ambao tutautumia kesho kama inavyopaswa kwa mujibu wa kanuni kwakuwa hatujafanya mazoezi ya mwisho hapo.

Back to homepage
Share this story