Wachezaji wote 19 waliosafiri kutoka jijini Dar es Salaam wameshiriki mazoezi hayo na hakuna yeyote aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kukosa mchezo wa kesho.
Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja amejitahidi kufanya jitihada mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi kesho.
Advertisement
Wachezaji wapya Ismael Sawadogo, Jean Baleke na Mohamed Mussa wameonesha kuwazoea wenzao haraka pamoja na mazingira licha ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa siku chache.
Tutaingia katika mchezo wa kesho kwa lengo moja la kupambana kupata pointi tatu muhimu ugenini ingawa tunajua itakuwa mechi ngumu.