Kiungo mkabaji Taddeo Lwanga, ameweka wazi furaha yake ya kurejea uwanjani baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu.
Taddeo raia wa Uganda amesema majeraha aliyopata ni makubwa na anajisikia furaha kurejea kuisaidia timu hasa kipindi hiki kwenye michuano ya kimataifa na ligi ya ndani.
Nyota huyo ameongeza kuwa kwa sasa mashabiki watarajie kumuona uwanjani siku za karibuni kwa sababu yuko fiti hivyo benchi la ufundi likiamua kumpa nafasi yuko tayari.
"Nilipata majeraha Oktoba mwaka jana katika mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy, jeraha lilikuwa kubwa namshukuru Mungu nimepona na nipo tayari kurudi uwanjani na mashabiki watarajie kuniona karibuni.
"Mimi kwangu najisikia furaha kucheza na yeyote katika eneo la kiungo mkabaji awe Jonas Mkude, Sadio Kanoute au Mzamiru Yassin kocha atakayeona anafaa kutokana na mechi husika," amesema Taddeo.