Ntibanzonkiza amesema jambo la muhimu ni kuisaidia timu kupata ushindi na kucheza vizuri ikitokea amefanikiwa kupata kiatu cha dhahabu itakuwa jambo jema na la furaha.
Ntibazonkiza amefikisha mabao 15 ya ligi mpaka sasa akizidiwa moja na kinara Fiston Mayele huku mchezo mmoja ukiwa umebakia.
"Namshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kupata ushindi mnono. Kwangu Simba ndio kitu cha kwanza kuhusu, kuibuka mfungaji bora itakuwa ziada ingawa nitafurahi ikitokea," amesema Ntibazonkiza.
Advertisement
Ntibazonkiza amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano kwenye mchezo mmoja katika historia ya ligi ya Tanzania.
Ntibazonkiza pia ameweka rekodi nyingine ya kufunga hat trick 2 katika msimu mmoja.