Mo amesema miongoni mwa sababu iliyotufanya kupata nafasi hiyo ni kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa katika miaka minne iliyopita, uwekezaji uliofanyika pamoja na mashabiki wanavyojitokeza kwa wingi uwanjani.
Mo pia amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kesho kuipa sapoti timu katika mchezo dhidi ya Raja Casablanca huku mwenyewe akisema atakuwepo uwanjani.