Simba Sports Club
News

VIDEO: Lukula aelezea mipango yake baada ya kutua Simba Queens

3 Oct 2022

Lukula amesema atatumia uzoefu alio nao kuisaidia timu kufanya vizuri kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itafanyika nchini Morocco Novemba mwaka huu.

Lukula ameongeza kuwa anafahamu uwezo wa kikosi tulicho nacho hasa baada ya kuwafunga katika Michuano ya CECAFA iliyofanyika hapa nchini Agosti mwaka huu akiwa na kikosi cha SHE Corporate ya Uganda.

Advertisement

"Kwanza naushukuru uongozi wa klabu kwa kuniamini na kunipa jukumu hili huku tukiwa tunaelekea kwenye michuano mikubwa Afrika.

"Sijaletwa hapa kwa bahati mbaya bali ni uwezo na uzoefu nilio nao katika kazi, kikubwa nahitaji ushirikiano kutoka wachezaji ili kukamilisha malengo tuliyojiwekea," amesema Lukula.

Back to homepage
Share this story