Simba Sports Club
News

VIDEO: Kocha wa Viungo afunguka baada ya mazoezi ya leo

14 Jul 2023

Hategekimana amesema mazoezi ya asubuhi yalikuwa ni kutaka kuona wachezaji wakicheza mpira uwanjani pamoja na kutengeneza nguvu baada ya jana kufanya mazoezi ya kuweka miili sawa.

Hategekimana amesema jioni wamefanya mazoezi ya nguvu na kuweka vizuri miili ya wachezaji ambapo kesho dozi itazidi kuongezeka ukilinganisha na jana na leo.

Advertisement

"Tulienda kwenye bwawa la kuogelea kwa ajili ya kuweka miili na misuli ya wachezaji kwenye hali nzuri ndio maana kulikuwa na maji ya moto kiasi."

"Tulitaka wachezaji wasahau mazoezi ya siku mbili za kwanza kwani kuanzia sasa kila siku ugumu wa mazoezi utakuwa ukiongezeka hadi kwenda kipindi cha mwisho wa maandalizi haya," amesema kocha Hategekimana.

Back to homepage
Share this story