Ahmed amesema tangu kikosi kimeondoka Lindi mchana njiani kimepata shangwe ya kutosha kutoka kwa mashabiki lakini baada ya kufika Mtwara shamra shamra zilikuwa kubwa zaidi.
Ahmed ameongeza kuwa mapokezi tuliyopata baada ya kufika Mtwara yameongeza morali kwa wachezaji na wanajiona wana deni la kuwalipa furaha Jumapili.
Advertisement
"Tumefika salama Mtwara tayari kwa mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Azam, tumepata mapokezi makubwa na tuna deni la kuwalipa furaha kwa kuingia fainali Jumapili."
"Wachezaji wapo kwenye hali nzuri, leo asubuhi tumefanya mazoezi Uwanja wa Majaliwa na hakuna yoyote aliyepata maumivu kwahiyo kikosi kizima kipo tayari," amesema Ahmed.