Abel ambaye amechaguliwa mchezaji bora wa mchezo dhidi ya APR amesema akili yake siku zote ilikuwa ikiamini akipata nafasi atacheza vizuri na kutoa mchango mkubwa kwa timu.
Aidha Abel ameendelea kusema kuwa katika mechi ya mwisho katika uwanja wa Amaan wakati akiwa na timu ya Taifa Jang'ombe alikuwa mchezaji bora wa wa mechi kama alivyofanya leo.
Advertisement
"Siri ya kiwango changu kuwa bora ni kusikiliza maelekezo ya walimu na kujituma mazoezi ili muda wote niwe tayari kwa ajili ya kuisaidia timu," amesema Abel.
Mlinda mlango huyo ameongeza kuwa anaamini akipewa nafasi ataendelea kucheza na kufanya vizuri.