Simba Sports Club
News

Uzinduzi wa Hamasa mchezo dhidi ya Petro De Luanda Jumatano

17 Nov 2025

Ahmed amesema hamasa hiyo itafanyika Chanika Zingiziwa ambapo Msafara utaanzia Buguruni, Ukonga, Pugu mpaka Chanika.

Ahmed ameongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa mchezo huo tumewekeza nguvu kubwa kwenye hamasa ili kushawishi mashabiki kuja uwanjani kwa ajili ya kuwapa sapoti wachezaji lengo likiwa kupata pointi tatu muhimu nyumbani.

"Jambo tunalotaka ni kujaza uwanja wa Mkapa na kwa Simba hilo hatuna wasiwasi. Tutazunguka jiji la Dar es Salaam lote kuhamasisha mashabiki kununua tiketi, Siku hiyo asibaki mtu nyumbani sote twendeni uwanja wa Mkapa," amesema Ahmed.

Advertisement

Baada ya ufunguzi huo zoezi la hamasa litaendelea ambapo Novemba 20 tutakuwa maeneo ya Mbezi na Goba ambapo Msafara utaanzia Magomeni, Morocco, Mwenge, Mbezi, Goba hadi Mbezi.

Ahmed ameendelea kwa kusema kuwa "Novemba, 21 itakuwa siku ya kurudisha kwa Mwenyezi Mungu kama ilivyo kawaida yetu na kwenye hili tutakuwa na wenzetu wa Mo DewjiFoundation kwenda kutoa msaada kwenye kituo cha kutunza watoto yatima Al Zam kilichopo Temeke na baada ya hapo tutapiga biriani."

"Jumamosi Novemba, 22 ndio itakuwa funga kazi ya hamasa kwa kwenda Vikindu. Tunawatangazia watu wote wa Vikindu na maeneo ya karibu tukutane kwenda kukamilisha hamasa. Dhamira yetu ya makusudi tunataka kujaza Uwanja wa Mkapa na kujaza uwanja sio lele mama, hiyo kazi tunaiweza peke yetu ndio maana wengine wamekimbia," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story