Simba Sports Club
News

Usanase aibeba tena Simba Queens dakika za jioni

23 Jan 2026

Usanase amefunga bao hilo baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Alliance ambao walikuwa makini muda mrefu.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa Queens, Usanase pia alifunga bao pekee la ushindi dakika ya 93 kwa mkwaju wa penati baada ya Jentrix Shikangwa kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Mchezo wa leo ulikuwa mgumu huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku idara za ulinzi zikionyesha umahiri mkubwa.

Advertisement

Kocha Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Zainah Nandede na Elizabeth Wambui na kuwaingiza Zawadi Usanase na Janeth Nyagali.

Ushindi huu unaifanya Simba Queens kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu baada ya kufikisha alama 28 kufuatia kucheza mechi 10.

Back to homepage
Share this story