Simba Sports Club
News

Usalama siku ya mchezo ni asilimia 100

31 Mar 2022

Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha ulinzi ili kuhakikisha kila shabiki atakayekuja uwanjani anarejea salama nyumbani kwake.

Ahmed amesema mara kadhaa kumekuwa na vitendo vya uhalifu hasa nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini ulinzi umeimarishwa na mashabiki wote watakaokuja watarejea majumbani kwao salama.

"Kwanza niwatoe hofu mashabiki wetu ambao wamepanga kujitokeza uwanjani waje bila wasiwasi sababu ulinzi utakuwa umeimarishwa na kila mtu atakuwa salama. Wanasimba msiwe na hofu njooni Benjamin Mkapa," amesema Ahmed.

Advertisement

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Tanzania (TADU), Jaeka Mdami amesema daladala za kwenda sehemu yoyote jijini Dar es Salaam zitapatikana na nauli itakuwa ile ile ya kawaida.

"Kuhusu usafiri utapatikana nje ya uwanja wa Benjamin na daladala za kwenda sehemu yoyote Dar es Salaam zitapatikana kwa hiyo mashabiki msiwe na hofu ya usafiri," amesema Mdami.

Back to homepage
Share this story