Simba Sports Club
News

Uongozi wa Klabu waitembelea Simba Queens

7 Oct 2025

Moja ya sababu ya kukutana na Simba Queens ni kuwaeleza mipango na malengo ya klabu kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026.

Keshokutwa Alhamisi kikosi cha Queens kitashuka katika Uwanja wa KMC kuikabili Mashujaa Queens kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii ikiwa kiashiria cha kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Wanawake 2025/2026.

Mwenyekiti wa klabu, Murtza Mangungu amewasisitiza wachezaji na benchi la ufundi kuwa malengo yetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri ili kurejesha heshima yetu ambayo msimu uliopita tuliikosa.

Advertisement

"Simba ni timu kubwa na kila michuano inayoshiriki lengo la kwanza ni kutwaa ubingwa. Tumefanya mabadiliko makubwa ya kikosi kwakuwa malengo yetu ni kufanya vizuri na hilo mnapaswa kulijua," amesema Mangungu.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa klabu, Zubeda Sakuru amesema Uongozi una imani na matumaini makubwa na wachezaji pamoja na benchi la ufundi hivyo kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake ili kufikia malengo.

Back to homepage
Share this story