Simba Sports Club
News

U20 yatinga nane bora

25 Mar 2026

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu ingawa tulimiliki sehemu kubwa na kutengeneza nafasi nyingi.

Crispin Posta alitupatia bao la kwanza dakika ya 35 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona.

Dakika saba baadae Bashiru Kibaila alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Singida kuunawa mpira ndani ya 18.

Advertisement

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 50 kupitia kwa Ezekiel Obed baada ya mpira wa kona kuokolewa na mlinda mlango wa Singida kabla ya kumkuta mfungaji.

Ushindi huu umetupa tiketi ya moja kwa moja ya kutinga nane bora tukiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Dodoma Jiji.

Back to homepage
Share this story