Simba Sports Club
News

U20 yapangwa na Azam michuano ya TFF

29 Jan 2022 By simbasc 1,525 views

Timu yetu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 imepangwa kucheza na Azam katika mchezo wa Nusu Fainali ya Michuano ya Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF).

Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park uliopo Kidongo chekundu Jumatatu Januari 31, saa 10 jioni.

Advertisement

Mechi yetu dhidi ya Azam itatanguliwa na nusu fainali ya kwanza kati ya JKT na JMK ambao utaanza saa tisa alasiri siku hiyo hiyo ya Jumatatu.

Kikosi chetu kimepata nafasi hiyo baada ya kushinda mechi zote nne katika hatua ya makundi ambapo ilishinda dhidi ya JKU, Ashanti, Cambiaso na JKT.

Back to homepage
Share this story