Mchezo huu kwetu ni wakuweka heshima kwa sababu hatuna nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua inazofuata katika mashindano haya.
Hatuna cha kupoteza kwenye mchezo huo bali tumejipanga kuhakikisha tunashinda tena kwa kuonyesha soka safi ili kuwapa furaha mashabiki wetu.
Kocha Barker atoa ahadi kwa mashabiki....
Kocha Mkuu, Steve Barker ameweka wazi wakati akiongea na Vyombo vya Habari kuwa leo ni mchezo wa kuweka heshima mbele ya mashabiki kwa kutandaza soka safi na kupata ushindi.
Barker ameongeza kuwa pia atautumia mchezo wa leo kuendelea kuimarisha kikosi chetu ambacho maendeleo yake ni mazuri hasa wachezaji wapya.
"Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mchezo pamoja na kuonyesha soka safi, tutautumia pia mchezo huu kuimarisha kikosi chetu ambacho maendeleo yake ni mazuri," amesema Barker.
Mwalimu nae atoa ya moyoni.....
Mshambuliaji, Seleman Mwalimu amesema tumekuwa na muendelezo mzuri katika mechi zetu za ligi zilizopita na tunataka kuendeleza ili kurejesha imani na matumaini kwa mashabiki.
"Tunahitaji kushinda mchezo wa leo ili kurejesha imani na matumaini kwa mashabiki wetu kuelekea katika michuano ya Ligi Kuu pamoja na CRDB Federation Cup," amesema Mwalimu.
Kapombe, Gueye kuwakosa Malien....
Nahodha wa timu Shomari Kapombe na kiungo mshambuliaji, Libasse Gueye hawatakuwa sehemu ya mchezo wa leo kwa sababu wanatumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Wawili hao waliionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Petro De Luanda ugenini ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao moja.