Tumefanikiwa kufika hatua hii baada ya ushindi wa jumla wa mabao 2-1 dhidi ya Gaborone United ya Botswana.
Mchezo wa kwanza ugenini Jumamosi iliyopita tuliibuka na ushindi wa bao moja na leo tumetoka sare ya kufungana bao moja.
Advertisement
Kwa upande wa wapinzani wetu Nsingizini wao wamefika hatua hiyo baada ya kuitupa nje Simbabhora ya Zimbabwe kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia sare ya bao moja waliopata mchezo wa kwanza.
Mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa kati ya Oktoba 17 hadi 19 nchini Eswatini wakati mechi ya marudiano itapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya Oktoba 24 hadi 26.