Simba Sports Club
News

Tutakutana na mshindi kati ya Uhamiaji na Libya 1 Kombe la Shirikisho Afrika

11 Jul 2024

Simba ni miongoni mwa timu ambazo hazitaanzia hatua ya awali bali itasubiri hadi hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mshindi kati ya Uhamiaji na Libya 1 tutakutana nae katika mchezo wa hatua ya kwanza kati ya Septemba 13-15 na marudio yatakuwa kati ya Septemba 20-22.

Advertisement

Katika mchezo huo tutaanzia ugenini kwenye mechi ya mkondo wa kwanza na marudiano tutakuwa nyumbani.

Mshindi wa jumla katika mchezo wa hatua ya kwanza atafanikiwa kupata tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Back to homepage
Share this story