Simba Sports Club
News

Tutakutana na Al Ahly Tripoli Kombe la Shirikisho Afrika

24 Aug 2024

Mchezo huo utakuwa wa ugenini ambao utapigwa nchini Libya kabla ya mechi ya marudiano ambayo itapigwa jijini Dar es Salaam, kati ya Septemba 20 hadi 22.

Al Ahly Tripoli imefika hatua hiyo baada ya kuitoa Uhamiaji kutoka Zanzibar kwa jumla ya mabao 5-1.

Advertisement

Sisi ni miongoni mwa timu chache zenye pointi nyingi Afrika ambazo hazikuanzia hatua ya awali.

Mshindi wa jumla kati yetu na Al Ahly Tripoli ataingia moja kwa moja katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Back to homepage
Share this story