Kikosi kinatarajia kurejea nchini kesho kutoka Mali na moja kwa moja kitaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi dhidi ya Mbeya City.
Mchezo dhidi ya City utapigwa Alhamisi, Disemba 4 katika Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo saa moja usiku tukiwa sisi wenyeji.
Advertisement
Mechi ya pili itakuwa dhidi ya Azam FC ambayo itapigwa Disemba 7 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni.
Baada ya mechi hizo ligi itasimama kwa mwezi mzima kupisha michuano ya AFCON ambayo itaanza kutimua vumbi Disemba 21 nchini Morocco.