Simba Sports Club
News

Tupo tayari Namungo FC Leo

19 Apr 2026

Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 tuliopata dhidi ya Fountain Gate kwenye mechi yetu iliyopita.

Tunafahamu itakuwa mechi ngumu na tunataraji kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga na tupo tayari kupambana mpaka mwisho ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea ya kupata alama tatu.

Barker akiri ugumu dhidi ya Namungo.......

Kocha mkuu, Steve Barker ameweka wazi kuwa haitakuwa mechi rahisi ndio maana amewaandaa wachezaji kuhakikisha tunacheza vizuri ili kuweza kupata alama tatu muhimu ugenini.

Barker ameongeza kuwa baada ya timu kufika Ruangwa jana wachezaji wamefanya mazoezi mwisho na wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo.

"Tumejipanga kuendelea kucheza soka safi na kupata alama tatu kwenye mchezo wa leo, ni wazi haitakuwa mechi nyepesi lakini tumejiandaa kwa hilo. Tunawaheshimu Namungo lakini dhamira yetu ushindi," amesema Barker.

Maandalizi yamekamilika......

Mlinzi wa kushoto, Anthony Mligo amesema pamoja na ugumu na upinzani ambao tunatarajia kukutana nao kutoka kwa Namungo lakini tumejipanga na tupo tayari kupambana mpaka mwisho ili kupata alama tatu.

Advertisement

"Tunaamini tunaenda kukutana na mechi ngumu, Namungo ni timu imara ina wachezaji wazoefu pamoja na kocha bora, lakini tutaingia uwanjani kwa mpango mzuri tutakaolekezwa na walimu, tunawaahidi mashabiki wetu kupata alama tatu muhimu ugenini," amesema Mligo.

Kapombe, Kagoma warejea kikosi....

Nahodha wa timu, Shomari Kapombe na kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma wamerejea kikosini baada ya kukosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Fountain Gate siku ya Alhamisi.

Wawili hao walikuwa wanatumikia adhabu ya kadi nne za njano na leo wapo tayari kuipigania timu mbele ya Namungo.

Kibabage, Kante kuikosa Namungo

Mlinzi wa kushoto, Nickson Kibabage ataukosa mchezo wa leo kwasababu ya kupata maumivu ya mguu.

Kwa upande wa kiungo mkabaji, Allasane Kante yeye ataukosa mchezo kwa sababu ya kuwa na kadi nne za njano.

Back to homepage
Share this story