Simba Sports Club
News

Tupo tayari kwa Mbeya Kwanza kesho

28 Jun 2022

Matola amesema hali ya hewa ni baridi lakini haitakuwa changamoto kwa kuwa tulianza kufika jijini Mbeya ambapo hakuna tofauti kubwa.

Matola amesema hautakuwa mchezo rahisi na anategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mbeya Kwanza lakini tumejipanga kuhakikisha tunaondoka na pointi zote tatu.

Advertisement

"Maandalizi yamekamilika, leo asubuhi tumefanya mazoezi ya mwisho na wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa kesho.

"Mchezo utakuwa mgumu najua Mbeya Kwanza watataka kupata ushindi hata kama wameshuka lakini sisi tunahitaji kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu," amesema Matola.

Back to homepage
Share this story