Pointi tatu katika mchezo wa leo ndio jambo pekee ambalo tunalihataji kuliko chochote.
Tunafahamu ushindi kwenye mchezo wa leo utatuweka kwenye mazingira mazuri katika mechi yetu ya pili inayofuata ambayo itakuwa ugenini.
Kocha Cadena atoa neno........
Kaimu Kocha Mkuu, Daniel Cadena amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo na hakuna kingine kinachohitajika zaidi ya ushindi.
Cadena amesema hali ya wachezaji ipo vizuri na wameshiriki vema mazoezi ya mwisho na hakuna aliyepata majeraha ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa leo.
"Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, hali za wachezaji zipo vizuri morali ipo juu, naamini kikosi chetu kitatupa matokeo chanya kesho," amesema Cadena.
Wachezaji wanaitaka mechi......
Mlinzi wa Kati, Che Fondoh Malone amesema wachezaji wapo tayari kupambana ili kuisaidia timu kupata ushindi.
Malone amesema kila mchezaji anahitaji kuwepo kwenye kikosi cha leo ili kuonyesha mchango wake kwa timu kupata ushindi.
Mara ya mwisho tuliwapiga 3-1 kwa Mkapa
Mara ya mwisho tulipokutana na ASEC Mimosas katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ilikuwa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo tuliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Katika mchezo huo uliopigwa Februari 13 mabao yetu yalifungwa na Pape Sakho (bao la tiktak lililoshinda tuzo ya bao bora Afrika). Mengine yalifungwa na Shomari Kapombe kwa mkwaju wa penati na Peter Banda.