Simba Sports Club
News

Tupo tayari kuwapa furaha Wanasimba Leo

1 Feb 2026

Ni mchezo muhimu kwetu ambao tunahitaji alama tatu pekee ili kurejesha matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hii.

Uongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wote kwa pamoja tumedhamiria kuwapa furaha Wanasimba ambao wanaitegemea.

Barker ana matumaini na jeshi lake...

Kocha Mkuu, Steve Barker ameweka wazi anakiamini kikosi chake na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri kuipambania timu mpaka tone la mwisho.

Barker amesema tuna faida kubwa ya kucheza mbele ya mashabiki wetu na wachezaji wapo kamili ingawa tunakutana na mpizani mgumu.

Barker ameongeza kuwa ushindi dhidi ya ES Tunis ndio jambo pekee ambalo tumejipanga kulifanya kwakuwa malengo yetu ni kufuzu hatua inayofuata.

"Tunajua tuna faida nzuri ya kucheza mbele ya mashabiki wetu lakini tunapaswa kuwa makini na kujitoa kwa asilimi 100 ili kupata ushindi dhidi ya ES Tunis Kesho. Ninawaamini wachezaji wangu na wapo tayari," amesema Barker.

Advertisement

Wachezaji wanaitaka mechi.....

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Morice Abraham amesema morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja anajua umuhimu wa ushindi katika mchezo huo.

"Morali zipo juu na kila mchezaji anajua umuhimu wa ushindi kwenye mchezo huu ndio maana hakuna maelekezo mengi, ushindi ndio kitu ambacho kipo vichwani mwetu," amesema Morice.

Jospin Loemba kuonekana kwa mara ya kwanza leo

Kiungo mpya Inno Jospin Loemba anatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza akiwa na jezi yetu tangu ajiunge nasi kutoka Colombe Sportive ya Cameroon wiki iliyopita.

Nyota mwingine Anicet Oura ambaye kwenye mchezo wa ugenini nchini Tunisia wiki iliyopita hakuwepo nae atakuwa sehemu ya kikosi cha leo.

Back to homepage
Share this story