Ni mchezo muhimu kwetu ambao tunahitaji alama tatu pekee ili kufufua matumaini ya kusonga mbele.
Tunafahamu tupo katika mazingira magumu ya kufuzu hatua inayofuata lakini hatujakata tamaa tutapambana mpaka mwisho kuona tutafanikiwa kuvuna nini.
Hiki ndicho alishosema kocha Barker..
Kocha Mkuu, Steve Barker amesema tuna wajibu wa kucheza soka safi na kupata matokeo ambayo Simba pamoja na mashabiki wetu tunastahili.
Barker ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu kutokana na mpizani wetu yupo nyumbani lakini hata hivyo tupo tayari kupambana.
"Utakuwa mchezo mgumu, tunaenda kukutana na mpizani mgumu lakini tunapaswa kupambana ili kupata matokeo ambayo mashabiki wa Simba wanataraji kuyapata," amesema kocha Barker.
Wachezaji hawajakata tamaa....
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Neo Maema amesema matokeo pekee ambayo tunayahitaji ni kupata alama tatu katika mchezo huu ingawa haitakuwa kazi rahisi.
"Wachezaji wote tupo tayari kwa mchezo, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tunahitaji matokeo ya alama tatu pekee," amesema Maema.