Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa tunafahamu utakuwa mgumu kutokana na ubora wa Azam lakini tumejipanga na tupo tayari.
Mchezo wa leo ni 'Dabi ya Mzizima' na mara zote unakuwa na upinzani wa asili na tupo tayari tumejipanga kuhakikisha sisi ndio tunafurahi baada ya filimbi ya mwisho.
Matola akiri ugumu wa Mzizima.......
Kocha Seleman Matola ameweka wazi kuwa benchi la ufundi pamoja na wachezaji wanafahamu ugumu wa mchezo huo kutokana na ubora wa Azam pamoja na kocha wao.
"Kwa ujumla kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tumejiandaa kimwili na kiakili kupambana dhidi ya Azam na malengo yetu ni kupata alama tatu."
"Tunafahamu haitakuwa mechi rahisi Azam wana timu nzuri wakiwa na kocha bora lakini tumejipanga na tupo tayari kuwakabili," amesema kocha, Matola.
Wachezaji wapo tayari kwa Dabi ya Mzizima....
Nahodha wa timu, Shomari Kapombe amesema licha ya ubora walionao Azam lakini tupo kuhakikisha tunapambana mpaka mwisho ili kuhakikisha tunapata ushindi.
"Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu, sote tunafahamu Azam ni timu nzuri lakini tumejipanga na tupo tayari kuwakabili na kupata alama tatu muhimu nyumbani," amesema Kapombe.
Tunataka kuendeleleza ushindi wa asilimia 100....
Timu yetu ndio pekee imeshinda kwa asilimia 100 katika mechi zote nne za mwanzo za Ligi Kuu ya NBC mpaka sasa na tunataka kuendelea hivyo.
Baada ya mechi za leo Ligi itasimama kupisha michuano ya AFCON ambayo itaanza kutimua vumbi Disemba 21 nchini Morocco na malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda na leo ili kuendelea kuweka rekodi ya asilimia 100.