Simba Sports Club
News

Tupo tayari kuikabili TRA United

9 Apr 2026

Tutaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya sare ya bila kufungana tuliopata ugenini dhidi ya Azam FC Jumapili iliyopita.

Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kwakuwa TRA ni timu imara inayoundwa na nyota wenye uzoefu pamoja na kocha bora mwenye uzoefu.

Barker atoa ya moyoni.......

Kocha Mkuu, Steve Barker amesema ni mchezo muhimu kwetu kupata alama tatu ili kuendelea kupigania mbio za ubingwa ingawa tunaamini haitakuwa kazi rahisi kutokana na ubora wa TRA.

Barker ameweka wazi kuwa ugumu mwingine ambao tutakutanao ni kwakuwa siku chache zilizopita tulipocheza dhidi yao tuliwafunga hivyo kesho nao watataka kulipa kikosi.

"Tupo tayari kwa mchezo, tunajua haitakuwa mechi rahisi hasa kutokana tumetoka kucheza nao siku chache zilizopita lakini tupo tayari," amesema kocha Barker.

Advertisement

Abel afunguka hali halisi ya mchezo.....

Kwa upande wake mlinda mlango, Hussein Abel amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na wataingia kwenye mchezo kwa lengo moja la kutafuta alama tatu.

"Sisi wachezaji tupo tayari, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tupo hapa kupambana mpaka mwisho kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu," amesema Abel.

Mpanzu kuikosa TRA......

Kiungo mshambuliaji Elie Mpanzu hatakuwa sehemu ya mchezo wa leo lichakuwa amefanya mazoezi pamoja na wenzake baada ya kutoka kwenye majeraha.

Kocha Mkuu Steve Barker amesema Mpanzu anaendelea kupata utimamu wa mwili na atakuwa tayari kuikabili Dodoma Jiji siku ya Jumapili.

Back to homepage
Share this story