Ni mchezo muhimu kwetu ambao tunahitaji matokeo chanya hasa baada ya kupata kupoteza mechi ya kwanza nyumbani.
Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka Stade Malien kutokana na uimara wao huku ikichangiwa nakuwa nyumbani kwao lakini tumejipanga kuwakabili.
Alichosema Kocha Matola kuelekea mchezo wa leo.....
Kocha Msaidizi, Seleman Matola ameweka wazi kuwa tumepata muda wa kuwatazama Stade Malien mechi yao ya kwanza ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika waliocheza dhidi ya ES Tunis ya Tunisia.
Matola amesema Stade Malien ni timu imara hasa wanapokuwa nyumbani lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ingawa tunafahamu itakuwa mechi ngumu.
“Ni mechi ngumu na zaidi sababu tunacheza ugenini, tuliangalia mechi yao ya kwanza ni timu nzuri lakini tumejiandaa kufanya vizuri na tunaamini tutaondoka na ushindi, wachezaji wetu wote wapo tayari kwa mchezo wa leo," amesema Matola.
Wachezaji wote tayari.......
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mkabaji, Allasane Kante amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na kila mmoja yupo tayari kuipigania timu kupata matokeo chanya.
“Tumekuja hapa Mali kucheza tukiamini tutafanya vizuri, tumekuja tukijua umuhimu wa mchezo huu sababu tulishapoteza katika mchezo uliopita hivyo tumejiandaa kupata matokeo mazuri,” amesema Kanté.