Simba Sports Club
News

Tupo tayari kuikabili Singida Black Stars

11 Mar 2026

Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya B19 katika mchezo wa hatua ya 32 ya CRDB Federation Cup tuliopata wiki iliyopita.

Ni mchezo mgumu ambao tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka Singida Black Stars lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.

Barker atoa kauli..........

Kocha mkuu, Steve Barker amesema mipango ya timu ni kuhakikisha tunacheza soka safi na hatimaye kupata alama tatu muhimu ugenini.

Akizungumzia hali ya kikosi, Barker amesema wachezaji wote 25 tuliosafiri wote wapo kwenye hali tayari kwa mchezo wa kesho tukiwa na malengo ya kupambana hadi mwisho ili kupata alama tatu.

"Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Singida lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho ili kupata matokeo chanya," amesema Barker.

Advertisement

Wachezaji wapo tayari kwa mchezo......

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mkabaji, Daud Semfuko amesema nyota wote wapo tayari kufuata maelekezo watakayopewa na walimu ili kufikia malengo tuliyojiwekea ya kupata alama tatu ugenini.

"Sisi kwetu kila mchezo ni muhimu wa kutafuta alama tatu, tunajua tutaenda kukutana na mpizani mgumu lakini tupo tayari kuhakikisha ushindi unapatikana," amesema Semfuko.

Tutacheza Airtel kwa mara ya kwanza......

Mchezo wa leo utakuwa wa kwanza kwetu kucheza katika Uwanja mpya wa Airtel tangu uzinduliwe mwaka jana baada ya kukamilika.

Back to homepage
Share this story