Simba Sports Club

Tupo tayari kuikabili Namungo FC

2 Nov 2026

Leo saa moja usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja Uhuru Dar es Salaam kuikabili Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Ni mchezo mgumu ambao tunataraji kukutana nao kutokana na ubora wa wapinzani wetu ambao tunaamini wapo kwenye hali nzuri.

Nafasi za timu zote kwenye msimamo....

Tupo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC tukiwa na alama 27 baada ya kupata ushindi kwenye michezo yote tisa tuliyocheza tukiwa na ushindi wa asilimia 100.

Kwa upande wapinzani wetu wapo nafasi ya saba kwenye msimamo wakiwa na alama 15 baada ya kucheza mechi 10.

Tulivyokutana mara ya mwisho....

Mara ya mwisho tulivyokutana na Fountain Gate ilikuwa Aprili 19 mwaka huu katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi tuliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Mchezo huo mabao yetu yalifungwa na Libbase Gueye, Anicet Oura na Elie Mpanzu wakati lile la Namungo lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Heritier Makambo.

Advertisement

Hali za Kikosi.....

Kocha wetu msaidizi, Seleman Matola ameweka wazi mbele ya vyombo vya Habari kuwa wachezaji watakaosekana ni wale majeruhi wa muda mrefu kama Wilson Nangu, Abdulazak Hamza na mlinda mlango Yakoub Suleiman lakini wengine wote tayari.

Kwa upende wa wapinzani wetu Namungo kocha mkuu, Juma Mgunda yeye amesema atamkosa nyota wake Gamba Matiko ambaye alipata maumivu kwenye mchezo uliopita lakini wengine wote wapo tayari.

Wachezaji wakuchungwa.....

Libbase Gueye, Anicet Oura, Elie Mpanzu na Clatous Chama ni nyota ambao wanatatajiwa kuendelea kuwasumbua nakuwa changamoto kubwa kwa walinzi wa Namungo.

Kwa upande wapinzani wetu nyota wao wa kuchungwa ni Herbert Lukindo, Pius Buswita na Rashid Chambo.

Matarajio ya jinsi mechi itakavyokuwa......

Katika mchezo wa leo kocha mkuu, Steve Barker hatarajiwi kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake kama ilivyo kawaida yake.

Hali hiyo hiyo inatarajiwa kwa kocha wa Namungo, Juma Mgunda.