Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate uliopigwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa umemalizika kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja
Mchezo ulianza kwa kasi huku tukishambulia na kufika zaidi langoni mwa Fountain Gate lakini mlinda mlango, Machupa Kapili alikuwa kikwazo kikubwa.
Nahodha Rushine De Reuck alitupatia bao la kwanza dakika ya 33 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Nathaniel Chilambo.
Kipindi cha pili Fountain Gate walirudi kwa kasi huku walionyesha dhamira ya kutaka kurudisha bao hilo lakini tulikuwa imara kudhibiti mashambulizi yote.
Ushindi huu unatufanya kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha alama 27 kufuatia kucheza michezo tisa.
X1: Kapili, Mukombozi, Awara, Obasi (Kindemile 85') Haruna (Juma 45'), Sadik (Mey 88'), Pandu, Obadia, Mgunda, Ahmad, Ntambi (Seif 45')
Walioonyeshwa kadi:
X1: Kassali, Chilambo, Mligo, Toure, De Reuck, Kagoma, Gueye (Chama 75'), Maema (Jabaar 75'), Mpanzu, Morice (Makgalwa 56'), Oura (Mgunda 88')
Walioonyeshwa kadi: Obina 31' Mgunda 41' Mukombozi 45+2'