Simba Sports Club
News

Tupo tayari kuikabili Mbeya City

4 Dec 2025

Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa tunafahamu utakuwa mgumu na tunatarajia kupata upinzani mkubwa ingawa malengo yetu ni alama tatu.

Mara zote tunapokutana na City mchezo huwa unakuwa mgumu lakini wachezaji wetu wameandaliwa kimwili na kiakili kuhakikisha ushindi unapatikana.

Alichosema Kocha Matola......

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema tunatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa City hasa ukizingatia wametoka kufanya mabadiliko katika benchi lao la ufundi lakini tumejipanga na tupo tayari kuwakabili.

Matola ameongeza kuwa wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na jana walifanya mazoezi ya utimamu wa mwili na leo watafanya mazoezi ya mwisho tayari mchezo huo.

Advertisement

"Kwa upande wetu tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunafahamu itakuwa mechi ngumu kwakuwa timu zote zimejipanga ila tutapambana hadi mwisho ili tupate ushindi," amesema Matola.

Wachezaji wapo tayari......

Nae mlinzi wa kulia, David Kameta 'Duchu' amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na wapo tayari kwa ajili ya kupambania alama tatu nyumbani.

"Sisi wachezaji tupo tayari kufuata maelekezo tutakayopewa na benchi letu la ufundi lengo likiwa ni kuhakikisha alama tatu za nyumbani zinapatikana," amesema Duchu.

Back to homepage
Share this story